Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Buigiri iliyopo Chamwino Dodoma kushirIki katika futari aliyowaandalia watoto hao, Machi 24, 2025. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na watatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari aliyowaandalia Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wenye Mahitaji Maalum, Buigiri iliyopo Chamwino Dodoma, Machi 24, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watoto katika futari aliyowaandalia Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wenye Mahitaji Maalum, Buigiri iliyopo Chamwino Dodoma, Machi 24, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Stanley Keneth (mwenye ulemavu wa macho) wa Darasa la Sita katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Buigiri ya Chamwino Dodoma katika futari aliyowaandalia wanafunzi hao, Machi 24, 2025. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)