Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Maafisa na Askari wa JWTZ jijini Mbeya leo tarehe 26 Machi 2025.
Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya Ulinzi.
Aidha,amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakuwa salama wakati wote.
Nishani hizo ni Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema,Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ na Nishani ya Jumuiya ya SADC.