*DC Chikoka asisitiza utunzaji wa miundombinu ya umeme
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Juma Chikoka amewapongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kuendelea kuhamasisha matumizi bora ya nishati kwa Watanzania wote.
Mhe. Chikoka amebainisha hayo leo Machi 27, 2025 kwa Wataalam wa REA waliofika kujitambulisha ofisini kwake kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya REA mkoani Mara.
Aidha, ameiomba REA kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu gharama za kuunganisha umeme, utunzaji wa mazingira, tahadhari za umeme na elimu kuhusu utunzaji wa miundombinu ya umeme ili kupata umeme wa uhakika.