Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amehitimisha zoezi la uvishaji nishani kwa kuwavisha Nishani mbalimbali Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Mtwara leo tarehe 28 Machi 2025.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Shughuli za Rais,Sura ya 9,Toleo la Urekebu la mwaka 2002 alitunuku nishani mbalimbali ambapo Jenerali Mkunda amevalisha nishani hizo kwa niaba yake.
Miongoni mwa waliovishwa nishani hizo leo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Michael Mangwela Mntenjele .
Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia Taifa kwenye nyanja ya Ulinzi.
Aidha,amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakuwa salama wakati wote.
Nishani hizo ni Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema,Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ na Nishani ya Jumuiya ya SADC.