Leo tarehe 29.03.2025, wananchi wa Mtaa wa Mwaja, Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki zoezi la usafi wa Mazingira wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa lengo la kuweza mazingira safi kwa ajili ya afya zao.
Usafi huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwaja, Athumani Makuka ambaye aliambatana na Afisa Mtendaji wa Mtaa, Mwanaasha Mani.
Zoezi hilo la usafi lilifanyika katika mtaro unaopita pembezoni mwa Shule ya Msingi Chinangali ambao umehusisha kuzibua mtaro wenye urefu wa mita 100 sambamba na kutoa taka ngumu kama makopo na mifuko kwenye mtaro huo ili kuruhusu maji yaliyotuwama kwa sababu ya mvua kutiririka pasina kizuizi chochote.