Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda (wa kanza kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Moshi Kabengwe wakati akitoa msaada wa mahitaji ya vitu mbalimbali leo Machi 29, 2o25, Dar es Salaam katika Kituo cha Kulea watoto ya Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni Mikumi, Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akimpa zawadi mtoto anaishi katika kituo cha Umra Orphanage Center kwa ajili ya Sikukuu ya Eid el Fitri na Pasaka.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA Bw. Richard Kayombo (wa kwanza kulia) akiwa na Naibu Mkurugenzi Utawala na Rasilimaliwatu TRA Bw. Nahoda P. Nahoda wakikabidhi mahitaji katika kituo cha Mother of Mercy Children’s Home kilichopo Madale, Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Uhusiano kwa Umma TRA Rachel Mkunda akizungumza jambo katika hafla fupi ya kutoa msaada wa kutoa mahitaji katika Kulea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Umra Orphanage Center.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa msaada wa mahitaji ya vitu mbalimbali katika vituo vya Kulea watoto ya Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni Mikumi na Mother of Mercy Children’s Home kilichopo Madale, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuonesha mshikamano na kurudisha kwa jamii pamoja na kuwatakia kheri ya Sikukuu ya Eid el Fitri na Pasaka.
Akizungumza leo Machi 29, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mahitaji katika kituo cha Kulea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Umra Orphanage Center, Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda, amewapongeza wasimamizi wa vituo kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwalea watoto.
Mwenda amesema kuwa katika mikoa 26 wamechangua maeneo yenye uhitaji kama njia ya kurudisha kidogo katika jamii katika kanda zote ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kuonesha kwamba TRA ni sehemu ya jamii.
“Kazi mnayofanya Serikali inapaswa kufanya kwa kuwezeshwa kwa kila mtanzania kuchangia kwa kulipa kodi na kufanikiwa kuisaidia jamii ikiwemo kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, TRA inahusika na matatizo ya jamii ndiyo maana leo tupa hapa ”amesema Mwenda.
Amesisitiza muhimu wa kila mtu kuichangia serikali kwa kulipa kodi jambo ambalo litasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuisaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.
Kamishna Mwenda amehaidi kuchangia shilingi milioni nne ili kusaidia upatikanaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto wa kituo Umra Orphanage Center, huku akitoa wito kwa watoto wa kituo hicho kuongeza juhudi katika masomo ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kufika ndoto zao.
Katika hatua nyengine Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA Bw. Richard Kayombo, akishirikiana na Naibu Mkurugenzi Utawala na Rasilimaliwatu TRA Bw. Nahoda P. Nahoda wamekabidhi mahitaji kituo cha Mother of Mercy Children’s Home kwa ajili ya maandalizi ya kusherekea sikukuu ya Eid el Fitri na Pasaka.
Akizungumza na watoto wa Kituo cha Mother of Mercy Children’s Home Bw. Kayombo amewatia moyo watoto wa kituo hicho katika kuhakikisha wanapiga hatua za mafaniko katika maisha yao, huku akieleza kuwa TRA itaendelea kuwa pamoja nao wakati wote.
Naye, Muasisi wa Kituo cha Umra Orphanage Center Rahma Kishumba na msimamizi kituo cha Mother of Mercy Children’s Home Christina Christopher wameishukuru TRA kwa kuwapatia msaada wa mahitaji kwa ajili ya watoto na kuwatakia mema katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.