Na Chedaiwe Msuya, WF, Mwanza.
Serikali
kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi
wa makundi mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza, hatua inayolenga
kuwawezesha kujenga misingi imara ya kifedha kwa maendeleo endelevu.

Wajasiriamali
wa Kata ya Misungwi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, wameelezea
shukrani zao kwa Serikali kwa kuwawezesha kupata elimu ya fedha
iliyotolewa na maafisa kutoka Wizara ya Fedha katika ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, yamewapa mwanga wa kupanga na
kuimarisha ustawi wao wa kifedha.

Mafunzo
hayo yamewalenga wajasiriamali, watumishi , wanafunzi, na wafugaji,
yakiwa na dhima ya kuwawezesha kusimamia fedha zao kwa ufanisi, kuepuka
mikopo umiza, na kujiandaa kifedha kwa maisha ya baadaye, ikiwemo
kipindi cha kustaafu.

Kwa
niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Misungwi, Afisa Sheria Bw.
Steven Singila alisisitiza kuwa elimu ya fedha waliyoipata imewajengea
uelewa wa umuhimu wa kujiwekea akiba, uwekezaji, na maandalizi ya maisha
ya baadaye.

“Tunaomba
pia tuendelee kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali ili tuweze kuboresha
miradi yetu na kujiandaa kwa maisha baada ya kustaafu. Kupitia elimu
hii, tumejifunza kuwa hata kama kipato ni kidogo, bado kuna njia sahihi
za kuweka akiba na kuwekeza kwa faida endelevu,” alisema Bw. Singila.

Aidha,
Bi. Lucy Mbarika, kwa niaba ya washiriki wengine, alieleza kuwa elimu
waliyoipata itawawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kifedha, kuepuka
madeni yasiyo na tija, na kutumia taasisi rasmi za kifedha kwa mikopo na
uwekezaji.

“Mafunzo
haya yametufungua macho kuhusu masuala ya kifedha, tumejifunza jinsi ya
kupanga bajeti, kutenga akiba, na kuepuka madeni yasiyo ya lazima elimu
hii itatusaidia sio tu kama wajasiriamali, bali pia kama familia na
jamii kwa ujumla,” alisema Bi. Lucy.

upande wake, Afisa Mkuu Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya
Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, alibainisha kuwa
mwitikio wa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza umekuwa
wa kuridhisha.

“Tunaipongeza
jamii kwa mwamko wao wa kutaka kujifunza na kutumia elimu ya fedha kwa
ufanisi, tumejifunza kutoka kwa washiriki na maoni yao yatazingatiwa
katika awamu zijazo za utoaji wa elimu ya fedha ili kuhakikisha
inawafikia watu wengi zaidi,” alisema Bw. Kimaro.

ya elimu ya fedha ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa
wananchi wanakuwa na uelewa sahihi wa masuala ya kifedha ili kuboresha
maisha yao, kukuza uchumi wa kaya, na kupunguza utegemezi wa kifedha
kupitia matumizi sahihi ya rasilimali walizonazo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Steven Singila, akizungumza na
Timu ya Wataalam ya kutoa Elimu ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha na
Taasisi zake, walipofika Ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa elimu ya
fedha ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa
makundi mbalimbali katika Kata ya Misungwi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa
Mwanza.

Afisa Usimamizi wa Fedha
Mwandamizi kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha,
Bw. Salim Khalfan Kimaro, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na
umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa Huduma Ndogo za Fedha na vile vya
kijamii kwa wananchi wa Kata ya Misungwi, kwenye program maalum ya elimu
ya fedha iliyotolewa kwa wananchi katika ukumbi wa Halmashauri ya
Misungwi Kata ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya wajasiriamali na
wananchi kutoka Kata ya Misungwi Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza,
wakiwa pamoja na Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya
Fedha na Taasisi zake Wilayani humo, wakichangia mada mbalimbali kuhusu
elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu yenye maudhui kuhusu
matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza,
umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa
fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye
masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na
mali nyingine.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Mwanza)