Zaidi ya Waumini mia tatu wa Dini ya Kiislamu wamehudhuria Iftar Maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi iliyofanyika nyumbani kwake Iwambi Jijini Mbeya.
Katika hotuba yake ya ukaribisho ambapo Mgeni rasmi alikuwa Sheikh Msafiri Njalambaha, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amemshukuru kwa kuitikia wito ulitolewa muda mfupi kutokana na majukumu ya kazi.
Sheikh wa Mkoa Msafiti Njalambaha ameshukuru kupokea mwaliko huo uliotolewa na Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi hasa Iftar hiyo iliyoandaliwa nyumbani inakamilisha thawabu mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kukarimu wageni.
Kutika hatua nyingine Sheikh Msafiti Njalambaha ameipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Sheikh Dour Mohammed mbali ya kushukuru hafla hiyo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kumwamini Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi katika nafasi mbalimbali katika Wizara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Edina Mwaigomole ameshukuru kushiriki hafla hiyo inaonesha upendo wa dhati ulioneshwa na Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi.