Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Kemirembe Lwota amekabidhi Mkono wa Eid kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kituo cha kulelea watoto waliokimbia kukeketwa cha Hope for girls and women Tanzania ambapo amesema Serikali itahakikisha inakemea na kuchukua hatua Dhidi ya wanaojihusisha na Vitendo vya Ukatili.
Kemirembe amekipongeza kituo hicho kwa namna kinavyolea watoto hao nakupambana na vitendo vya Ukatili ikiwemo ukeketaji pamoja na Vipigo ambao amesema kamwe Serikali haitavumilia kuona Vitendo hivyo vikiendelea kushamili katika jamii anayoiongoza.
“Niwapongeze hope kwa Kazi kubwa mnayoifanya Serikali itaendelea kuwaunga Mkono katika mapambano haya lakini niwataka wananchi wa Serengeti vitendo hivi vikome Kabisa natuwe sehemu ya kutoa Taarifa tubapobaini”Alisema Kemirembe Lwota Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.
Kwa upande wake Daniel Misoji ambaye nimsimamizi wa kituo hicho ameongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwakukumbuka kituo hicho kutokana na umhimu wake ambapo amesema wanajibika kwa kiasi kikubwa katika kuwahudumia watoto ambao wanatoka katika Mazingira magumu.