Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga, kimetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wanakikundi hao wametoa msaada huo leo Aprili 1, 2025, wakiongozwa na Mwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali hiyo.
Dkt. Tizeba amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia watoto njiti, lakini pia vifaa vingine vitahusiana na mradi wa ushonaji waliouanzisha katika hospitali hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kijasiriamali akina mama waliojifungua watoto njiti wakati watoto wao wanaendelea kupatiwa huduma za kiafya hospitalini.
“Team March tumeanzisha mradi wa ushonaji wa kofia, masweta, soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti. Tunataka kuwawezesha akina mama hawa kwa kuwapa ujuzi wa ushonaji ili waweze kujiinua kiuchumi, huku wakiendelea kutunza watoto wao hospitalini,” amesema Dkt. Tizeba.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, amepokea msaada huo na kuwashukuru wanakikundi kwa kujitolea kuokoa maisha ya watoto njiti.
“Tunaipongeza ‘Team March’ kwa juhudi zao kubwa za kusaidia watoto njiti. Mmeacha alama kubwa katika hospitali hii. Tunawashukuru kwa namna mnavyoguswa na afya za Watanzania na tunawaomba wadau wengine waendelee kutembelea hospitali hii na kusaidia changamoto zinazojitokeza,” amesema Dkt. Luzila.Mwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo vilivyotolewa na Team March.
Picha na Na Kadama Malunde – Malunde 1 blogMwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila (kushoto) vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo vilivyotolewa na Team March
