Selcom Tanzania na Bahati Nasibu ya Taifa wameanzisha ushirikiano mpya wenye lengo la kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa michezo ya bahati nasibu kwa Watanzania. Ushirikiano huu utatoa fursa kwa watumiaji kufika kwa urahisi na kwa usalama, huku ikiwezesha mfumo wa malipo wa Selcom kufika kwa washiriki wote.
Mkurugenzi wa ITHUBA, Bwana Kelvin Koka, alieleza kuwa kupitia muunganiko huu, watafanikisha upatikanaji wa huduma ya Bahati Nasibu ya Taifa kwa kutumia USSB Code, hivyo kuwezesha watanzania kushiriki kwa njia rahisi na salama.
Aidha, Selcom Tanzania, kupitia msimamizi wa kitengo cha masoko, Shumbana Waluawa, walisisitiza kwamba wana mtandao mkubwa wa mawakala nchini kote, hivyo kuleta huduma hii karibu na kila mtanzania.
Wamesema kuwa mtandao wao unatoa urahisi katika zoezi la kuhamisha pesa kutoka benki au kupitia mifumo ya simu, hivyo kuwezesha wananchi kushiriki katika michezo ya bahati nasibu bila vikwazo. Ushirikiano huu utasaidia kuongeza ufikivu na usalama katika huduma ya bahati nasibu, na kutoa fursa kwa wateja wengi zaidi.
Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya michezo ya kubahatisha, ambapo washiriki sasa wataweza kushiriki kwa njia za kisasa na salama, Selcom na ITHUBA wameonyesha dhamira ya kuleta mabadiliko makubwa kwa kutoa huduma bora na kwa urahisi, huku wakihakikisha kuwa huduma hizi zinawafikia watanzania wote bila kujali mahali walipo.
Kwa kuunganisha mifumo ya malipo na miundombinu ya usalama, ushirikiano huu utaongeza ushiriki wa wananchi katika michezo ya bahati nasibu, hivyo kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi.