Wadau wa madini wameendelea kuvutiwa na madini yanayowasilishwa katika Kituo Cha Jemolojia Tanzania (TGC) jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mnada wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika Aprili 08, 2025.
Katika hatua nyingine, wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kurejesha minada ya madini nchini.