Na Mwandishi wetu.
WANAFUNZI wanaotajia kumaliza kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Mzumbe wameaswa kujiamini kwa sababu wamejianda vizuri kufanya mtihani wa Taifa mwaka huu.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi waliosoma Mzumbe Sekondari (Mzumbe alumin) Edward Talawa ameyazungumza hayo shuleni hapo Mzumbe Mkoani Morogoro wakati akiongea na wanafunzi hao wanaotarajia kumaliza kidato cha sita shuleni hapo.
Amesema wanapoenda kufanya mtihani wajue kila kitu kinawezekana, na wanabahati wako kwenye shule yenye vipaji na kufundishwa na walimu waliobobea.
“Tunaimani mtaleta matokeo mazuri, tuna Alumn ambayo sasa imetimiza miaka kumi na nyie kama wahitimu wa Mzumbe Sekondari tungependa mjisajili” alieleza.
Aidha Talawa amewaanbia wanafunzi hao kuwa wanaposoma waangalie mwelekeo wa uchaguzi wako, ili waweze kupata kipato cha kuweza kujiendeleza, ni vyema kuwe na chanzo cha kipato zaidi ya kimoja.
“Usione kwamba huwezi unaweza endelea kujituma, kunakuanguka sana ili kufikia mafanikio hivyo misukosuko ni sehemu ya maisha,” alisema Talawa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Alumin Mkata Nyoni ameeleza kwamba kuendelea na masomo ya juu ni kwenda kujijenga zaidi katika mafunzo ya kitaaluma.
“Sasa hivi mnaenda kukutana na jamii mjitahidi kuwa na uwezo wa kufanya vitu ili muwe sehemu ya jamii bora, hivyo basi msiingie katika mkumbo wa kukariri vitu, mnauwezo wa kujiajiri na kufanya vitu mnavyotaka,” alieleza.
Awali Mjumbe wa Alumin SACP (RTD) Jamal Rwambow amewambia wahitimu hao kutoka kata tamaa, ingieni kwa nguvu zote mkiongozwa na nidhamu katika kutafuta fursa za uchumi.
Naye Katibu wa Alumin ya Mzumbe Collis Rutenge amesema kuzaliwa maskini sio kosa lako ila kufa maskini ni kosa lako kwa sababu ya maamuzi unayoyafanya na kazi unayoyafanya na weledi wako.
“Katika Maisha ya uhalisia soma taaluma yoyote, na usichague kazi, watoto wako wanataka kuona unawasaidia kufikia malengo yao”.
Katika mjadala huo Mwanafunzi Jameson Katimos amesema kukutana na Mzumbe Alumin kumewasaidia kujifunza na kutuongezea Imani tunaweza kufanya vizuri.
“Tumekutana na wanafunzi wa zamani wa Mzumbe ambao wanamitizamo tofauti ya kujenga kuhusu namna ya kukabiliana na maisha na wamefahamika kwakufanya vitu vikubwa”