Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Rashid All Salim, akimkaribisha Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, mara baada ya kufika, Ofisini kwake visiwani Zanzibar, kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa visiwani humo kwa utaratibu wa PPP.

Naibu Katibu Mkuu, Uchumi na Uwekezaji, Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Rashid All Salim, (wapili kulia, mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha Tanzania Bara, Bw. Bashiru Taratibu, (Katikati, mstari wa mbele), Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor Khatib, (wapili kushoto, mstari wa mbele) pamoja na Timu ya Wataalam wa PPP Zanzibar na Tanzania Bara, kabla ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa visiwani humo kwa utaratibu wa PPP.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Rashid All Salim, akiagana na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, walipomaliza kufanya mazungumzo, Ofisini kwake visiwani Zanzibar, kabla ya Timu ya Wataalam wa PPP pande zote mbili (Tanzania Bara na Visiwani), kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa visiwani humo kwa utaratibu wa PPP.

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa visiwani Zanzibar, kwa utaratibu wa PPP.

Washiriki wa kikao kuhusu Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, na Wizara ya Fedha, Tanzania Bara, wakifuatilia wasilisho katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa ZURA, mjini Zanzibar, kilichohusisha watumishi wa kitengo na Idara ya ubia katika Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa pande zote mbili, kikiambatana na ziara ya Timu ya Wataalam wa PPP kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Zanzibar kwa utaratibu wa PPP.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Rashid All Salim, akijadiliana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, kuhusu miradi inayotekelezwa Visiwani Zanzibar, kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), wakati wa Kikao kuhusu Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar na Wizara ya Fedha, Tanzania Bara, katika Sekta ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kilichofanyika katika Ukumbi wa ZURA visiwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akimsikiliza Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, wakati akifafanua jambo baada ya kikao kuhusu Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar na Wizara ya Fedha, kilichofanyika katika Ukumbi wa ZURA Visiwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, (wakwanza kulia, walioketi), na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Rashid All Salim, (Katikati, walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalam wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Tanzania Bara na Zanzibar.


Picha za matukio mbalimbali ya washiriki wa Kikao cha Pili kuhusu Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, na Wizara ya Fedha, Tanzania Bara, kilichofanyika katika Ukumbi wa ZURA, visiwani Zanzibar. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF- Zanzibar)
……..
Na Asia Singano, WF – Zanzibar.
Wataalam wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi nchini, wameagizwa kuhakikisha miradi yote mikubwa yenye mvuto wa kibiashara nchini inatekelezwa kwa njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili kukuza uchumi wa nchi.
Agizo hilo limetolewa Visiwani Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi Amina Khamis Shaaban, wakati akifunga Kikao cha Pili kuhusu Ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar na Wizara ya Fedha, Tanzania Bara, katika masuala ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kilichofanyika katika Ukumbi wa ZURA visiwani humo.
Alisema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Sekta Binafsi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, elimu na huduma nyingine zote muhimu kwa ubora na urahisi na kukuza uchumi wa nchi.
‘’Ni muhimu kushirikisha sekta binafsi katika mipango ya maendeleo, ambao wao wana ujuzi wana utaalamu lakini vilevile wengine wana fedha kwa hiyo hilo ni jambo muhimu katika kushirikiana nao’’ alisema Bi. Amina.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Rashid Ali Salim, ameitaka Sekta Binafsi nchini kutumia fursa zilizopo Serikalini za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwakuwa pande zote mbili zitanufaika na fursa hizo.
‘’Tunaialika Sekta Binafsi kuja kuwekeza katika miradi hii ambayo ina manufaa makubwa mbali na ajira na kulipa kodi, miradi hii hurejeshwa Serikalini baada ya muda tutakaokubaliana kwa mujibu wa mkataba” alisema Bw. Salim.
Naye, Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, alisema Wizara ya Fedha, kupitia Kitengo cha PPP, itaendelea kuungana kwa pamoja na Idara ya PPP Zanzibar, kuendelea kushawishi Sekta Binafsi kushirikiana na Sekta ya Umma kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
‘’Ahadi yetu sisi ni kushirikiana na wenzetu hawa kuhakikisha kuwa tunatengeneza mazingira mazuri yatakayowezesha kuvutia sekta binafsi kuja kuungana na Serikali zetu zote mbili kuhakikisha tunatekeleza miradi hii ya maendeleo’’ alisema Bw. Taratibu.
Hiki ni kikao cha Pili cha mashirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Kikao cha kwanza kilifanyika Desemba mwaka wa fedha 2024/2025, huku Kikao kinachofuata kikitarajiwa kufanyika mwaka ujao wa fedha.