Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) leo Aprili 8, 2025 akiwa katika kikao na Menejimenti ya Wizara ya Maji mahususi katika kufanikisha kazi ya kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi na namna bora zaidi ya kupata majibu ya kuondosha changamoto zinazojitokeza katika kuwahudumia wananchi.
Waziri Aweso amesisitiza kwamba watendaji wa Wizara ya Maji hakuna kulala na wafanye kazi usiku na mchana katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo la “kumtua mama ndoo ya maji kichwani” unaendelea vyema bila kuchoka na kuhakikisha kutekeleza malengo ya serikali ya kuhakikisha huduma ya maji inapatikana mijini kwa asilimia 95 na kwa vijijini asilimia 85.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri akizingumza kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara amesema watendaji wamepokea maelekezo yote na wapo tayari kuyafanyia kazi.