Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni na kufanya naye mazungumzo kwenye Viwanja vya Ikulu ya Uganda.
Akiwasilisha ujumbe huo, Mhe. Kikwete ameelezea uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda, na dhamira ya Mhe. Rais Samia ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Kwa upande wake, Rais Museveni amepongeza uongozi thabiti wa Mhe. Rais Samia, si tu ndani ya Tanzania bali pia katika Bara la Afrika kwa ujumla.
Ameeleza furaha yake kwa kumkaribisha Rais Mstaafu wa Tanzania katika Ikulu ya Uganda na kusisitiza kuwa Tanzania ni mfano bora wa uongozi wenye utulivu na demokrasia imara barani Afrika.