.jpg)

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT).
Mhe. Khamis amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo tarehe 9 Aprili, 2025 wakati akijibu swali la Mhe. Bakar Hamad Bakar (Baraza la Wawakilshi) aliyetaka kujua kwa kiasi gani Zanzibar inanufaika na fedha zitolewazo na Wadau wa maendeleo kupitia Serikali ya Muungano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Akiendelea kujibu swali hilo, Mhe. Khamis ameeleza kuwa kupitia fedha hizo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na SJMT imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ametaja miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume Pemba, Barabara ya Tunguu hadi Makunduchi, Chakechake hadi Wete kupitia kwa Binti Abeid na ujenzi wa Skuli, Hosptali na Masoko.
Amesema miradi inayotekelezwa Zanzibar imewasaidia wananchi wa pande zote mbili za Muungano kushiriki na kuinua hali zao za kiuchumi pamoja na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
”Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 imeweka utaratibu wa namna SMZ inavyopaswa kunufaika na mikopo, dhamana na misaada kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.
Pamoja na kupongeza hatua ya Serikali ya kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha hizo, Mhe. Bakar katika swali lake la nyongeza alitaka kujua kama Serikali haioni haja ya kupitia na kuboresha utaratibu mpya kwa mgawanyo wa fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Katika majibu ya Serikali, Naibu Waziri Khamis amesema utaratibu wa mgawanyo wa fedha upo kwa mujibu wa sheria na umewek wazi kuwa Zanzibar inanufaika kwa asilimia 4.5 na Tanzania Bara asilimia 95.5.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha Muungano unaendelea kuwa imara Serikali zote mbili zimekuwa zikifanya vikao bado vikao vinakaliwa ili kuna namna ya kuboresha kuhakkikisha.