Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe akikabidhi jiko sanifu linalotumia nishati safi ya umeme mara baada ya kufunga Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini leo tarehe 12 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe wakati akifunga Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini leo tarehe 12 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Wataalamu wa mazingira kutoka mikoa na maafisa viungo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira
Bw. Juma Charles kutoka Sayari Safi akitoa maelezo kuhusu namna ya kutumia jiko sanifu kwa washiriki wa Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini leo tarehe 12 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mazingira kutoka mikoa mbalimbali mara baada ya Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini leo tarehe 12 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
……………..
Wataalamu wa mazingira katika mikoa yote nchini wametakiwa kuwa mfano na kuhamasisha na kusimamia matumzi ya nishati safi ya kupikia kwenye jamii.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe wakati akifunga Kikao Kazi cha Wataalamu wa Mazingira Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini leo tarehe 12 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Kikao hicho killichofunguliwa tarehe 11 Aprlli, 2025 kimekwenda sanjari na zoezi la kukabidhi majiko sanifu yanayotumia nishati safi ya umeme kwa wataalamu wa mazingira wa mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Akifunga kikao kazi hicho, Bw. Kavishe amesema ni wakati sasa kwa wataalamu hao kushikirikiana kwa pamoja na kufanyia kazi changamoto za kimazingira zilizoibuliwa na mikakati yake iliyowekwa vilete matokeo chanya katika nchi.
Bw. Kavishe amesisitiza wataalamu hao wa mazingira wa mikoa kuendeleza ushirikiano na maafisa viungo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi kwa ujumla kuhakikisha lengo la usimamizi wa mazingira linakuwa endelevu.
“Nina imani mtashirikiana katika kuhakikisha mnatoa elimu kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira, bustani za kijani, kutunza vyanzo vya maji, misitu, fursa zilizopo katika biashara ya kaboni, uchumi wa buluu na nishati safi,” amesema.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Mazingira Mkoa wa Mwanza Bw. Mangabe Mnilango amesema kikao hicho ni daraja kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais na wataalamu wa mazingira wa mikoa hiyo hivyo kufanikisha kazi ya kuratibu masuakla ya mazingira.
Aidha, amesema mkoa huo bado una changamoto ya magugu maji ambayo yameleta madhara katika sekta ya usafiri na mazingira na katika kukabiliana nayo tayari Serikali imeanza kufanyia kazi changamoto hiyo.
Pia, Bw. Mnilango ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi katika mkoa wake kufuga kisasa kwa kutokuwa na mifigo mingi katika eneo moja kwani haloi hiyo huharibu ardhi.
Naye Mtaalamu wa Mazingira wa Mkoa wa Mara Bi. Nawabi Miyola amewahasisha wanawake na wananchi kwa ujumla kutumia nishati safi ya kupikia ili kupunguza gharama na muda katika mapishii.
Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia husaidia wanawake kufanya majukumu mengine wakati wa kupikia badala ya kuzunguka kutafuta kuni kwenye misitu.
Vilevile, Bi. Nawabi ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwakabidhi majiko ya kisasa yanayotumia nishati safi ya umeme mdogo ambayo yatakuwa chachu kwao kuhamasisha wananchi.