Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo leo Aprili 12,2025 Dar es Salaam ambapo wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa uboreshaji wa Soko la Kariakoo ambalo ni la kimataifa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange (wa kwanza kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila wakati wa ukaguzi wa mradi wa Soko la Kariakoo leo Aprili 12,2025 ambapo amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 98 na kuwa soko hilo litafanya kazi kwa saa 24 za siku.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru akitoa maelezo kwa Wabunge kuhusu miundombinu ya Soko la Kariakoo leo Aprili 12,2025 walipokagua mradi huo. Kushoto kwake(aliyevaa tai) ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Justin Nyamoga akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa Soko la Kariakoo katika ukumbi wa Arnatouglo leo Aprili 12, 2025 Dar es Salaam ambapo ameshauri Serikali kuhakikisha wafanyabiashara wote wenye sifa wanarejeshwa kwa haki na usawa ili kuepusha malalamiko. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akitoa maelezo kwa wabunge kuhusu namna Serikali ilivyotekeleza mradi wa ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo na kwamba soko hilo litafunguliwa hivi karibuni ambapo mradi huo umegahrimu shilingi Bilioni 28.
Mwonekano wa juu wa Soko jipya la Kariakoo leo wakati Kamati ya Bunge ya TAMISEMI ilipokagua utekelezaji wa mradi huo ambapo imeridhishwa na jinsi serikali ilivyoboresha mazingira ya kufanya biashara.
(Habari na Picha na Shirika la Masoko ya Kariakoo)