Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma kwaajili ya kushiriki Kongamano la kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Tarehe 13 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma kwaajili ya kushiriki Kongamano la kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Tarehe 13 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 13 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 13 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo ya Uongozi Imara iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 13 Aprili 2025. (Anayekabidhi tuzo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi tuzo kwa Familia ya Baba wa Taifa iliyopokelewa na Edward Nyerere wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 13 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo ya usimamizi mahiri wa utunzaji mazingira iliyotolewa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 13 Aprili 2025. (Anayekabidhi tuzo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti)
………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere alisisitiza sana Watanzania kulinda amani na umoja katika nchi, aliamini kwa dhati usawa wa binadamu na ujenzi wa Taifa lisilo na matabaka.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 103 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma. Amesema Baba wa Taifa alikuwa pia muumini mkubwa wa maridhiano, ustahimilivu na ujenzi wa Taifa huru linalojitegemea na aliiongoza nchi kwa misingi hiyo.
Makamu wa Rais amesema kwa kuendeleza falsafa hizo ,Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimarisha amani na umoja wa kitaifa kupitia falsafa yake ya R4 iliyojikita katika kujenga upya, kufanya mabadiliko ya kisera, kiutawala na kimuundo, kujenga mapatano na maelewano pamoja na ustahimilivu. Ameongeza kwamba kupitia falsafa hiyo, Mheshimiwa Rais ameliwezesha Taifa kuimarisha umoja wa kitaifa, mshikamano, mifumo ya kitaasisi na kiuchumi na kupanua uhuru wa watu kufanya shughuli zao zikiwemo za kisiasa na kidini.
Aidha Makamu wa Rais amesema Mwalimu Julius Nyerere aliamini katika kujenga umoja miongoni mwa nchi za Afrika ambapo licha ya jitihada za kuunda Umoja wa nchi mbalimbali Afrika, pia kwa pamoja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume waliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema Baba wa Taifa alihimiza kuulinda Muungano wetu kwa nguvu zote na kuhakikisha kero zozote zinazojitokeza zinatatuliwa kwa njia ya mazungumzo na maridhiano ambapo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi ya kuimarisha tunu ya Muungano kwa kutatua hoja za Muungano, ambapo hadi sasa ufumbuzi wa jumla ya hoja 15 za Muungano umepatikana.
Makamu wa Rais amesema Serikali imeendelea kuenzi jitihada za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alitambua mapema umuhimu wa kuwa na miundombinu imara na aliwekeza katika ujenzi wa reli ya kati. Amesema kwa kauli mbiu ya “Kazi Iendelee” Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza mazuri yote ya viongozi waliomtangulia ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kimkakati ,kutanua fursa za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, kuboresha huduma za kijamii za afya, elimu na maji, kuvutia uwekezaji nchini na kukuza uhusiano wa kimataifa na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi.
Makamu wa Rais ameitaja miradi mikubwa iliyofanikishwa katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege, upanuzi wa bandari zetu, ujenzi wa meli, ujenzi wa barabara kuu na za vijijini, ujenzi wa hospitali za rufaa, mikoa na wilaya, pamoja na zahanati na vituo vya afya, ununzi wa vifaa tiba vya kisasa na kusomesha madaktari bingwa, na ujenzi wa miundombinu ya elimu msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki uchaguzi wa viongozi bora, akianzia na uchaguzi wa tarehe 1 Novemba, 1962 mara baada ya Tanganyika kupata uhuru. Aidha amesema alisisitiza ushiriki wa Wanawake katika chaguzi h ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefuata nyayo hizo kwa kuwashirikisha wanawake wengi zaidi kwa nafasi za juu serikalini katika uongozi wake.
Makamu wa Rais Amesema Wananchi wanaposhiriki kikamilifu katika uchaguzi, wanapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi yanayogusa maisha yao ya kila siku na hivyo kuimarisha uwajibikaji wa viongozi waliopo madarakani katika ngazi mbalimbali.
Vilevile Makamu wa Rais amewasihi vijana wa Tanzania kusoma zaidi vitabu kuhusu Baba wa Taifa ili waweze kujifunza maarifa na maono makubwa yaliyomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti ameiomba Serikali kuendelea kuimarisha Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili iendelee kuwa chombo cha kumuenzi kiongozi huyo na kusaidia kujenga umoja na mshimanao ikiwemo kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na umoja kama alivyoasa Baba wa Taifa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema tayari Wizara ya Maliasili na Utalii imepata kiwanja katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma kwaajili ya Ujenzi wa Makumbusho ya Marais.
Amesema ndani ya Makumbusho hiyo kutakuwa na sehemu ya kuonesha historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Kitaifa na Kimataifa. Aidha amesema eneo la Kongwa limetangazwa kuwa urithi wa Taifa kwa kutambua mchango wake katika kutumika na wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika.
Amesema Wizara itaendelea kushirikiana na wadau wengine kutangaza maeneo mengine ya kambi ambazo zilitumika na wapigania uhuru kutoka nchi za kusini mwa Afrika.