Na Mussa Makali
Mkurugenzi wa shirika la usambazaji umeme nchini (Tanesco) Mhandisi Eng Boniphace Gisima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kufuatia ajali iliyotokea wilayani Bunda mkoani Mara.
Akizungumza kwanjia ya Simu kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Pius Lutumo amesema tukio hilo limetokea majira kati ya sanane ,Satisa baada ya Dereva kumkwempa mwendesha Baiskel na kugongana na Lori uso kwa uso.
Kwa mujibu wa kamanda Lutumo Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha Dereva wake.
“Ni kweli tukio lipo na amefariki dunia yeye na Dereva wake baada ya kumkwepa mwendesha Baiskel na kugongana uso kwa uso na Lori”Alisema kamanda wa polis Mkoa wa Mara.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali Teule ya wilaya ya Bunda huku wakisubiri taarifa zaidi kuhusu taratibu zingine.