BABATI, MANYARA.
TIMU ya Polisi Tanzania Jumapili hii Aprili 13, 2025 inawakaribisha Cosmopolitan katika mchezo wa Ligi ya Championship, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mjini Babati.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Afisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro amesema kikosi hicho kipo vizuri na wachezaji wana ari na morali ya kuhakikisha kuwa wanapata alama tatu katika uwanja wao wa nyumbani ili kujihajikishia usalama wa kusalia katika ligi hiyo.
Amesema ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa lakini kwa upande wao wanaendelea kutoa ushindani ili kusalia na hatimaye kujipanga kwa msimu ujao.
Lukwaro amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwapa hamasa wachezaji waweze kufanya kazi yao vyema na kupata ushindi.
Mpaka sasa timu ya Polisi ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama 31 baada ya kucheza michezo 25