Lagos Nigeria – Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa MahusianowaBenki ya CRDB Bank, Tully Esther Mwambapa, ametajwa kuwa Kiongozi Anayeongoza kwa Uwezeshaji Barani Afrika (Iconic Empowerment Personality of the Year) katika hafla ya tuzo za Kutambua Wanawake Mashuhuri Barani Afrika (African Iconic Women Recognition Awards).
Katika hafla hiyo hiyo, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, ametunukiwa tuzo ya Heshima ya Kipekee kwa Uongozi wa Kiwango cha Juu Barani Afrika (Imperial Honour for African Iconic Global Leadership of the Year).
Hili ni tukio la kihistoria kwa Tanzania ambapowanawake viongozi wawili wametambuliwa kwa heshima za juu kabisa katika bara la Afrika siku moja. Huu ni ushahidi wa nguvu, ushawishi, na msukumo mkubwa wa wanawake wa Kitanzaniakatika jukwaa la kimataifa.
Tuzo ya Tully ni matokeo ya juhudi zake kubwakatika kuwawezesha wanawake na vijana kupitia programu jumuishi na bunifu za kifedha. Uongoziwake ndani ya CRDB Bank Foundation umebadilimaisha ya maelfu ya Watanzania, hususanwajasiriamali vijana na wanawake kupitia programu ya iMbeju, ambapo ndani ya mwaka mmoja tokeakuanzishwa kwake imefikia zaidi ya wanawake na vijana 800,000. Programu ya iMbeju inatoa mafunzo ya ujasiriamali, ushauri, elimu ya fedha, na mitaji wezeshi.
Tully ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika sektaya benki, ambapo amehusika katika kubuni bidhaa na huduma bunifu zilizochangia kupanua wigo wa ujumuishi wa kifedha nchini. Kupitia CRDB Bank Foundation, anaendelea kuwa chachu ya matumainina mabadiliko chanya katika jamii.
Tuzo hii imekuja katika kipindi cha kipekee ikiwa ni miaka 30 tangu Azimio la Beijing, mpango muhimuwa kihistoria wa kuendeleza haki na usawa wa wanawake duniani. Pia, tuzo hii imekuja wakatiBenki ya CRDB ikisherehekea miaka 30 tangukuanzishwa kwake, ikiwa ni taasisi ya kifedha inayozidi kuonesha dhamira ya dhati katika kuwawezesha wanawake.
Wakati dunia inatafakari mafanikio ya miaka 30 ya harakati za usawa wa kijinsia tangu Beijing, na wakati Benki ya CRDB ikisherehekea miongo mitatuya huduma kwa Watanzania, tuzo ya Tully inakuwaalama hai ya mafanikio haya. Kazi yake inaakisimalengo ya Azimio la Beijing katika kuondoavikwazo, kutoa fursa kwa wanawake, na kuinuajamii.
Tuzo hii pia inaipa Benki ya CRDB nafasi ya pekeeya kuwa miongoni mwa taasisi za kifedha barani Afrika ambazo haziegemei tu upande wa ujumuishwaji wa kifedha, bali pia zinakuwa mstariwa mbele katika kufanikisha usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu. Aidha, inadhihirisha falsafa ya kipekee ya CRDB Bank Foundation katika kutumiahuduma za kifedha kuchohea maendeleo ya kijamii, huku ikithibitisha kuwa benki inaweza kuwa na lengo la zaidi ya kutafuta faida, na kuwa chombo cha kusukuma mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Katika tuzo hii Tully ameibuka mshindi dhidi ya viongozi wengine wanawake mashuhuri barani Afrika ikiwamo Odunayo Sanya, Mkurugenzi Mkuuwa MTN Foundation, Balo Atta, Afisa Mtendaji Mkuu wa UBA Foundation), Osayi Alile Afisa Mtendaji Mkuu wa Aspire Coronation Trust Foundation), Somachi Chris-Asoluka, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tony Elumelu Foundation, na Claire Akamanzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Maendeleo Rwanda.
Ushindi wa Tully ni uthibitisho muhimu kuwawanawake wana nafasi muhimu ya kubadili maisha na kuchochea maendeleo katika jamii na Taifa.