Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kisongo Arusha na baadae alilkuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Chama cha Kisima Mafanikio lililofanyika kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Wa nne kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali alipotembelea banda la Maonesho la Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye Viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri , wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania ( BASATA) , Dkt. Kedmon Mapana na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za Maonyesho kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Lilian Shayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali alipotembelea banda la maonesho la Masai Market Arusha lililo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio lililofanyika kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto ni Flament Kivuyo na wa pili kushoto ni Sarah Robert wote kutoka Masai Market Arusha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Zaituni Iddi (kulia) ambaye ni mwanachuo wa fani ya Umeme wa Majumbani kutoka VETA Arusha, alipotembelea banda la maonesho la VETA kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wakiimba Wimbo wa Taifa wakati Waziri Mkuu alipofungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri. (Picha na Ofisi ya Wazri Mkuui)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipofungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua nembo ya Chama cha Kisima cha Mafanikio baada ya kufungua Kongamano la chama hicho kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejidhatiti kuendelea kukuza na kuimarisha sanaa nchini ikiwa ni moja ya sekta rasmi ya kiuchumi.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili (Aprili 13, 2025) katika Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania, linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha. Ambapo amesema fani ya ushereheshaji ni uchumi.
Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kaunzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao unakopesha hadi shilingi Milioni 100 kwa wasanii wakiwemo washereheshaji ili waweze kujiimarisha kimitaji na vitendea kazi.
“Pia kupitia maboresho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 yaliyofanyika mwaka 2022, Serikali imeanzishwa tozo ya hakimiliki (copyright levy) ambapo asilimia 60 ya makusanyo inakuja kwenu moja kwa moja na asilimia nyingine 10 inakuja kwenu kupitia Mfuko”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga Ukumbi wa Kimataifa ya Sanaa na Michezo ‘Arts and Sports Arena’ kwa shilingi bilioni 300. “Haya yote ni maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameaigiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana chama cha Kisima cha Mafanikio katika kuandaa miongozo, mafunzo ya kitaaluma, na mfumo wa urasimishaji wa washereheshaji nchini.
“Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) endeleeni kushirikiana na Kisima cha Mafanikio katika kukuza matumizi sahihi ya Kiswahili kwenye majukwaa mbalimbali”.
Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali inatambua kazi ya Chama cha Kisima cha Mafanikio. “Hakika kazi yenu ni ya msingi, nyeti na yenye mchango mkubwa kwa Taifa”.
Kwa Upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake mahiri na kwa kutoa fursa kwa watanzania kukuza vipaji vyao na kuendeleza stadi za kazi na taaluma katika tasnia mbalimbali ikiwemo ya ushereheshaji na upangaji wa matukio.
Hakika Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa katika mstari wa mbele wa kulea vipaji vyote na kuvipa nafasi kuweza kuonekana na kutenda kazi zao kama ilivyokwenu watu wa Kisima cha Mafanikio”.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Ester Kimweri ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoomgozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia uzalendo nchini.
“Sisi wadau wa sekta hii tunapenda kuonesha nia yetu ya dhati kuendelea kuunga mkono juhudi hizi kwa vitendo kwa kuuelimisha, kuuhamasisha, kuburudisha na kufundisha na sisi tutaendelea kuheshimu sheria, kulinda rasilimali, mali za umma, kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii”