Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Balozi Dkt. Stergomena Tax pamoja na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Balozi Dkt. Stergomena Tax pamoja na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo na Taifa la India kwa manufaa ya pande zote mbili. Amesema ziara aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India Oktoba 2023 imeimarisha zaidi uhusiano uliopo.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kushirikiana na Jamhuri ya India katika masuala ya Ulinzi ikwemo ziara za viongozi wa Wizara za Ulinzi kutoka pande zote mbili, ziara za Wakuu wa Majeshi pamoja na kubadilishana mafunzo mbalimbali.
Amepongeza ushirikiano na India katika zoezi la pamoja la kijeshi baina ya Tanzania, India na nchi washirika Afrika ambalo linahusisha jeshi la Wanamaji sambamba na maonesho ya zana na vifaa vya ulinzi. Makamu wa Rais ametaja maeneo mengine ambayo Tanzania imekuwa ikishirikiana na India katika masuala ya Ulinzi ikiwemo mafunzo ya pamoja ya kijeshi katika kudhibiti ugaidi, kupambana na uharamia, uokoaji na doria za pamoja.
Halikadhalika Makamu wa Rais amepongeza ushirikiano na India katika masuala ya Afya, Elimu, Maji, Usafiri na huduma zingine za kijamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya India Mhe. Sanjay Seth amesema katika Tanzania imeimarisha zaidi ushirikiano na Taifa la India na kuwa mshirika wa kuaminika katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo biashara, uwekezaji, maji, afya na elimu.
Mhe. Sanjay amesema Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa ufanyaji biashara na Jamhuri ya India ikitarajiwa kufikia dola bilioni nane kwa mwaka 2024/2025. Aidha ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuridhia kufanyika kwa mafunzo ya jeshi la Wanamaji na Maonesho ya zana na vifaa yanayofanyika nchini yakishirikisha Jamhuri ya India na nchi washirika Barani Afrika.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Balozi Dkt. Stergomena Tax, Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Bishwadip Dey pamoja na Viongozi mbalimbali wa Jeshi la Ulinzi kutoka Tanzania na India.