Na Silivia Amandius.
Kyerwa , Kagera.
Mkuu wa wilaya ya kyerwa Bi Zaituni Msofe amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Samia Suruhu Hassan kwa kuleta Kampeini ya msaada wa kisheria na kusema kupitia kampeini hiyo inaenda kuwa mkombozi katika halmashauri ya wilaya ya kyerwa kwani changamoto kubwa ni ya migogoro ya ardhi.
Akizungumza ofisini kwake wakati akipokea timu ya wataalamu wa msaada wa kisheria ambayo imehusisha wataalamu mbalimbali kama wataalamu wa dawati la jinsia polisi,maafisa ardhi,maafisa maendeleo ya jamii, mawakili wa serikali pamoja na wakili kutokaTLS amesema kyerwa inaenda kuwa ya tofauti kwani ofisi ya mkuu wa wilaya imekuwa ikipokea migogoro mingi sana kupitia kampeini ni hatua mojawao ambayo itakuwa halmashauri imepiga kwa kupunguza migogoro.
“Migogoro mingi ya huku inahusisha ardhi ambapo unakuta wanandoa wanagombania ardhi yaani shamba kwa ajili ya mavuno hasa ya kahawa kwani huku kilimo kikubwa ni kahawa kwahiyo tunashukuru sana Rais wetu Mama Samia kwani ametambua wananchi wake wengi awana uelewa wa sheria na kupitia kampeini hii tunaenda kuongeza uelewa kwa wananchi kwa asilimia kubwa na kuiona kyerwa mpya” amesema Dc Zaituni.
Aidha amewataka wananchi kutumia fursa hii kwani imekuja kwa ajili yao kupeleka mararamiko yao ili waweze kupatiwa ufumbuzi na kusema kuwa Kampeini hii itakuwa katika kata kumi na vijijini 30 ikiwa kila kata vitahudumiwa vijiji vitatu na kuwataka wananchi kutokuwa chanzo cha kutengeneza migogoro wenyewe .
Nae mratibu wa Kampeini hiyo katika halmashauri ya kyerw amabae pia ni wakili wa serikali kutoka wizara ya katiba na sheria Bi Kasilida Chimagi amesema lengo la Kampeini hii ni kuongeza uelewa kwa wananchi kwa ni msaada wa kisheria kwa watu wote na unatolewa bure.
Ameongeza kuwa endapo kesi aitaisha ndani ya siku kumi bado watabaki wataalamu wa Halmashauri ambao wapo katika idara ya katiba na sheria kupitia ngazi ya halmashauri watashughurikia mashauri hayo na kuhakikisha yanaisha kabisa.
“Kampeini hii itashughurikia masuala mbalimbali kama migogoro ya ardhi,kesi za madai na jina, haki za watoto,wakina mama, wazee na watu wenye ulemavu na migogoro mingine mingi na hii ni kutokana tunayo timu ya kutosha kwahiyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hii katika maeneo yao tutakayo yafikiw ndani ya siku kumi kwa ni timu imejipanga vizuri”amesemaa Bi Kasilida.