MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Bw.Charles Kichere,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasilisha ripoti yake ya Mwaka 2023/24 bungeni Dodoma.
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Bw.Charles Kichere,akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 16,2025 jijini Dodoma mara baada ya kuwasilisha ripoti yake ya Mwaka 2023/24 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKAGUZI na Mdhibitinwa Hesabu za Serikali(CAG), Charles Kichere ameliahauri Bunge kuona namna bora ya kuzijadili ripoti za mwaka 2023/24 mapema kabla ya Bunge kuvunjwa ili kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
CAG.Kichere ametoa Ushauri huo leo Aprili 16,2025 jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano wake wa uwasilishaji wa Ripoti za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha mwaka 2023/24.
Amesema walishaanza majadiliano na bunge ili kuona namna ya kuweka utaratibu wa kuanza kujadili ripoti hizo mapema zaidi kuliko hivi sasa ili ziweze kufanyiwa kazi zikiwa bado za moto.
“Mwanzo muda ulikuwa mrefu zaidi, ukapunguzwa na sasa tulishaanza majadiliano ipungue na ziwe zinajadiliwa mapema zaidi, nashauri ikimpendeza spika ripoti za mwaka huu zijadiliwe mapema zaidi kabla ya kuvunja bunge kuelekea uchaguzi mkuu,”amesisitiza Kichere.
Akizungumzia mzima ripoti ambayo ameziwasilisha CAG amesema kuwa amewasilisha ripoti 14 za ufanisi katika sekta mbalimbali huku aliwataka wanahabari na wananchi kwa ujumla kusoma ripoti hizo kupitia jarida Maalum lililoandaliwa na Tovuti ya CAG kwa makini na kuona mambo yanayotekelezwa na Serikali yao,l.
Kwa upande wake Mwenyekiti ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza amempongeza CAG kwa kuwa na timu nzuri ya wakaguzi ambayo inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa, hadi kufikia kupata kazi ya umoja wa mataifa na Tanzania kufanya ukaguzi wa kimataifa.