Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), Raymond Peter Mbilinyi pamoja na Mjumbe wa Bodi, Richard Raynerius Manamba, wakishiriki mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga yaliyofanyika leo, Aprili 16, 2025, nyumbani kwa marehemu eneo la Migungani, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) wakiongozwa na Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO CPA. Sadock Mugendi wameungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga yaliyofanyika leo, Aprili 16, 2025, nyumbani kwa marehemu eneo la Migungani, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.