Na Silivia Amandius.
Kyerwa, Kagera.
Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya kyerwa wameshauriwa kupeana ushirikiano katika kutatua migogoro ya ardhi hili kuepusha gharama za mashauri katika mabaraza ya ardhi na hata mahakamani.
Hayo yameelezwa na diwani wa kata kamuli mh. Jonas Twegumya Vedasto katika mkutano wa adhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi kamuli uliohusisha wananchi pamoja na wataalamu wa kampeini ya msaada wa kisheria ya mama samia ambapo amewaasa kutogombania maeneo yasiyo yao au kuwa na kawaida ya kushirikishana katika kutatua kero zao za mirathi na migogoro ya ardhi.
“Mama samia anatupenda mpaka kutuletea kampeni hii maana yake anajua wananchi wake huku ngazi ya vitongoji wanatakiwa kupata elimu ya sheria ili kuondokana na migogoro na kujenga Tanzania yenye amani na maendeleo kama kauli mbiu ya kama inavyosema MSAADA WA KISHERI KWA HAKI , USAWA, AMANI NA MAENDELEO” amesema Diwani Jonas.
Nae wakili kutoka katika chama cha mawakili wa kujitegemea Tanganyika TLS Ndg. Samwel Angelo amesema mashauri mengi ya ardhi mahakamani yanatumia gharama kubwa kutokana na wananchi kutoka maeneo ya vijijini ambapo utumia usafiri ambao upo juu zaidi.
“Tusitumie pia mabavu yetu kuwanyanyasa wasio na uwezo na kuwadhurumu mashamba yao au ardhi zao ila pia ukigombania hatua 3 za shamba mpaka kesi inafika mahakama ya rufani unajikuta unatumia gharama kubwa sana jambo ambalo mngekaa mkashauriana pande zote mbili na kumaliza mgogoro, tuache kutumia pesa bila mpangilio tunarudisha uchumi wetu chini hizo fedha tunazotumia kwenye mshauri ebu tuzitumie kutimiza matunzo ya familia zetu na mama Samia ameleta msaada huu wa kisheria kama elimu itakayowasaidia kupata uelewa “amesema wakili Samweli.
Nao baadhi ya wananchi wa kata kamuri akiwemo Bi. Sinforoza Cosma na bw. Tumuombe Fransis wameishukuru kampeini hiyo ya msaada wa kisheria kwani walio wengi wamekuwa wakikosa maalifa au uelewa wa sheria ya ardhi na mirathi ambayo upelekea migogoro ya ndoa na ardhi na pia wameomba baada ya kampeini hii kuisha uwepo mwendelezo wa kusikiliza na kutatua kero zao.
Sambamba na hayo wamesema licha ya mengi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita elimu ya mambo mengi imetolewa kwa asilimia kubwa na kupitia elimu hiyo ya msaada wa kisheria itaenda kuwa chachu pia ya kuimarisha maendeleo ya wilaya na hata ngazi ya chini ya vitongoji