Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe ametoa hadi Jumatano kwa nchi ya Afrika Kusini pamoja na Malawi kuondoa vizuizi vya mazao ya Tanzania kuingia katika nchi hizo,bila ya kufanya hivyo hakuna mazao yoyote ya nchi hizo mayo yatauzwa hapa nchini.
Bashe ameyazungumza hayo leo katika mkutano wa wadau wanaotekeleza miradi ya kuwawezesha vijana na wanawake katika sekta ya kilimo uliifanyika jana jijini Dodoma
Bashe amesema hakuna Zabibu zozote wala Apples pamoja na mazao mengine ambayo yanaletwa hapa nchini kutoka nchi hizo za Malawi na Afrika Kusini yataingia hapa nchini bila ya wao kuondoa vizuizi ili mazao ya Tanzania yaingie kuuzwa.
“We are not losers kwenye hili game,kama hawaondoi hakuna zao lolote la kwao litaingia hapa nchini,niwaambie tu wafanyabiashara kwenye hilo hakuna kitakachoendelea,”alisema Bashe.
Aidha amesema Serikali kupitia wizara ya kilimo,haijawahi kuzuia mazao ya nchi hizo kuingia hapa nchini sasa iweje wao wazuie mahindi kutoka Tanzania halafu wao wanyamaze kitu ambacho hajiwezekani.
Alifafanua zaidi ya kuwa hakuna mtanzania yoyote ambaye atapoteza maisha kwa ajili ya kukosa kula Apple la kutoka Afrika Kusini au Zabibu za nchi hizo wataendelea kutumia mazao ya hapa nchini.
Bashe amesema nchi haijawahi kumsumbua jirani yoyote kwenye soko la mazao,mara nyingi wakiwa na njaa wanapiga hodi na kusaidia sasa safari hii hakuna ndizi wala bidhaa yoyote ambayo itaingia hapa nchini.
Hata hivyo Waziri Bashe aliwapa pole wafanyabiashara wa hapa nchini kutokana na adha kubwa waliopata wakiwa na mizigo ya mazao ya mahindi kupeleka katika nchi hizo.
Alisema wasiwe na wasiwasi wowote kila kitu kitaakaa sawa na kuongeza kuwa safari hii hakuna bidhaa yoyote ya kilimo ambayo itapokelewa kama nchi hizo hazitafungua mipaka hiyo.