Na Ali I sssa Maelezo 17/4/2025.
Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Muhamed Ibrahim Sanya amesema vyombo vya habari nchini ni nguzo Muhimu katika kuleta maendeleo ya jamii na kuwepo uwajibikaji kwa uwazi wa shughuli zinazofanywa na Serikali na Mashirika ya umma katika ngazi za Taifa.
Ameyasema hayo leo huko Ofisini kwake Maisara Mjini Unguja katika mkutano na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Tuzo za Umahiri wa Mawasiliano kwa mara ya kwaza Zanzbar.
Amesema amefurahishwa sana kuona kuwa leo Zanzibar imezinduliwa Tunzo za Umahiri katika Mawasiliano ya Umma (Zanzibar Communication Excelence Award) ambazo zinalengo la kutambua na kuhamasisha wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari na mawasiliano wa Serikali na Mashirika ya Umma kwani wao ni watu muhimu na wana mchango mkubwa nchini katika kuiletea maendeleo kwa haraka.
“Leo ni siku ya furaha na historia kwa watu wote, bila shaka niko mbele yenu katika hafla muhimu ya uzinduzi wa tunzo za umahiri katika mawasiliano ya umma”, alisema Waheed Muhamed.
Aidha alifahamisha kuwa lengo kuu la tunzo hizo ni kutambua na kuhamasisha wadawu wa habari, maafisa habari wa mashirika na serikali wana nafasi kubwa kuielezea serikali yale mazuri yaliyotekelezwa kwa kipindi chote cha utawala wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussen Ali Mwinyi kwa kuandika Makala mbalimbali, habari, picha na katuni pamoja na kuandaa video.
Alisema tuzo hizo zitatoa hamasa kwa waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi kutoa taarifa za kina zenye ufanisi wa miradi ya serikali ya Zanzibar.
Aidha alisema pia tunzo hizo zitaweza kuinua mahusiano kwa kuunda jukwaa kati ya waekezaji na vyombo vya habari kwa kuongeza fursa za uekezaji, pamoja kuonesha fursa za kiuchumi, kutoa mafunzo kwa watendaji wa serikali, kuleta utengamano wa kijamii na mengineo.
Alieleza ofisi yake kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wana matumaini makubwa kuwa tunzo hizo zitaleta mapinduzi makubwa kwa maendeleo ya Zanzibar kupitia uchocheaji na utoaji wa taarifa sahihi na zenye weledi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Nae Mkururugenzi ya wa Institute of Public Reletion Tanzania (IPRT) Dr.Titus Solomon amesema tasisi yake tayari imeaza kutoa mafunzo hayo katika ngazi mbalimbali ya Jeshi la Polisi, ZRA, Chama cha walimu, Shirikisho la vyama vya ushirika na taasisi nyengine hapa nchini.
Mapema Mratibu wa Tunzo hizo Lufunyo Mlyuka alisema kuwa kuanzia mwezi Julai wwaka huu wanatarajia kutoa tunzo hizo zilizoshindanishwa ambapo wataaza kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari kabla ya kutoa tunzo hiyo.
Afisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Mwantanga Juma khamis akimuwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Salum Ramadhan aliwataka wandishi wa Habari kuichangamkia fursa hiyo ya Tunzo ya Umahiri kwani ni wakati kwao kufuatilia utekelezaji wa miraji ya maendeleo na kuandika habari ili kuitangaza kwa jamii.
“Waandae vipindi,wandike Makala na yote yale yanayo wahusu katika kazi zao”, alieleza.
Tunzo hizo zinafadhiliwa na Institute of Public Reletion Tanzania (IPRA), Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Wakala wa Bima Zanzibar ZIC Takaful, Zanzibar Communication Exelence Award (ZCEA) na Delaware Investment.




