Na Prisca Libaga RAS Arusha
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. DKT. Doto Mashaka Biteko amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mkalipa pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama Cha Mapanduzi leo tarehe 22 Aprili, 2025.
Dkt. Biteko yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 5 kutembelea na kukagua shughuli za miradi ya maendeleo kwenye Wilaya za Mkoa wa Arusha.





