Na Ashrack Miraji Fullshangwe Media
Wateja takribani 249 kutoka wilaya za Mwanga na Same wanaotumia hudums ya maji kutoka kwenye mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Same-Mwanga (SAMWASA) wanadaiwa zaidi ya shilingi million 200 na mamlaka hiyo ikiwa ni madeni ya Ankara (bili) za maji.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Same – Mwanga Mhandisi Rashid Shaban Mwinjuma amesema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto ya baadhi wateja takribani 249 wa wilaya ya same na Mwanga mkoani Kilimanjaro kutokulipa Ankara Cbill) za maji kwa wakati hali iliyosababisha mamlaka hiyo kudai zaidi ya milioni mia 200.
“Hali hii inatuathiri sisi mamlaka ya maji pale wananchi wanaposhindwa kulipa Ankara za maji kwa wakati, kwa hivi karibuni tumewaandikia barua wale wote tunaowadai, wanafikia 249 wa miji ya Same na Mwanga na wateja hawa tunawadai zaidi ya milioni 200, sasa hii fedha ni nyingi tukizikusanya kwa mara moja zinaweza kujenga mradi mpya, hivyo, tumeona si busara kwenda kusitisha huduma ya maji wa wadaiwa hao lakini tumeamua kuwaita ili tuzungumze tujue changamoto zao ni nini” alisema Mhandisi Rashid.
Mhandisi Rashid Ameongeza kuwa suluhu sahihi ya utatuzi wa changamoto hiyo ni kuzungumza na mteja ili kwa pamoja waweze kutatua changamoto hizo na kumfanya mteja aweze kupunguza deni lake ili huduma iendelee kuboreshwa zaidi kwa wateja waliofikiwa na miundombinu ya maji na wale ambao hawajafikiwa.
Ameeleza kuwa wateja wengi walifika ofisini kwao kwa ajili ya mazungumzo huku wengi wakieleza kuwa kuvuja kwa maji mbele ya mita, kuacha mabomba ya maji wazi bila uangalizi hali ambayo imepelekea maji kupotea na kusababisha bili kuwa kubwa kwa mtumiaji huku wengine madeni yao yakitokana na mlipaji kutoweka kwa namna mbalimbali ikiwemo kufariki, kuhama makazi au kusafiri kwa muda mrefu.
Pamoja na mambo mengine amewaomba wananchi na wateja wote wa Wilaya ya Same na Mwanga kuwa endapo kuna changamoto inayohusu huduma ya maji kufika ofisini kwa ajili ya mazungumzo na kuona njia sahihi ya kusaidiana pamoja na kuewa elimu ya matumizi sahihi ya maji ili kuepuka bili kubwa mwizo wa mwezi.
Mmoja ya wateja (jina lake ameomba lisitajwe) waliofika ofisini hapo ametuambia kuwa deni lake limekuwa kubwa kutokana na kuachwa kwa bomba wazi wakati maji yanapokuwa hayatoki, ameeleza kuwa maji yanapokuja kutoka huenda nyumbani kukawa hakuna mtu wa kufunga bomba hilo na kusababisha maji kutoka kwa muda mrefu zaidi ya masaa 7 hali iliyomsababishia kuwa na deni la zaidi ya laki moja na nusu kwa mamlaka ya maji.
Mwisho mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa dhamira ya mamlaka hiyo haiwzi kufikia malengo na mafanikio bila ushirikiano wa karibu kutoka kwa wateja na wananchi hususan katika swala la ulipaji wa Ankara za maji.