Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahim Juma akizungumza na Majaji wa mahakama ya rufani wakati akifungua kikao cha tathmini cha shughuli za mahakama kwa mwaka 2024. Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika katika ukumbi sa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Aprili 24, 2025.
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka Majaji wa Mahakama ya Rufani kujikita zaidi katika matumizi ya Teknolojia wigo wa matumizi ya teknolojia ili kupunguza mzigo wa mrundikano wa mashauri ya rufani mahakamani.
Profesa Juma ameyasema hayo leo Aprili 24, 2025 jijini Dar es Salaam katika kikao cha tathmini ya shughuli za Mahakama ya Rufani kuanzia Januari hadi Desemba 2024 kinachoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Amesema wakati wakiendelea kujipanga upya kuendelea kuondoa mlundikano wa mashauri katika Mahakama ya Rufani ni kuona haja ya kuchukua nafasi katika matumizi ya TEHAMA ili kuendelee kuboresha zaidi mfumo na kurahisisha utendaji kazi.
Amesema mahakama hiyo ina jumla ya majaji 39 na kwamujibu wa tathmini iliyofanywa na Mkuu wa kitengo cha tehma katika mahakama hiyo, kwa mwaka 2026 hadi 2030 kila jaji mmoja amekadiliwa uwezo wa kushughulikia mashauri ya rufani 99 kwa mwaka, sawa na rufani 3,861.
Amesema matumizi ya Tehama katika utoaji haki ni eneo muhimu ambalo halikwepeki na linahitaji tahadhari za kila mara kwasababu linabadilika badilika kila wakati.
“Ni muhimu wataalamu wa Mahakama wakaendelea kujifunza maendeleo yanayopatikana katika matumizi ya Teknolojia hasa ya Akili Mnemba (AI) katika utoaji wa haki ili Mahakama za Tanzania zivune manufaa makubwa kutoka katika matumizi ya hayo na kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kutokea.
Amesema, Teknolojia ni eneo ambalo hata Tanzania kama sehemu ya dunia haiwezi kukwepa isipokuwa kujipanga vizuri zaidi ili kuendelea kuitumia kwa faida,’’amesema Jaji Mkuu.
“Viongozi wa Mahakama ya Rufani tayari tumeona kuwa kiwango kidogo cha matumizi ya Teknolojia, hususani kwa njia ya mtandano ni ndogo mno ukilinganishwa na ngazi za chini za Mahakama hivyo kuna umuhimu wa kujitayarisha kufanya urekebishaji wa mchakato wa biashara na kuongeza matumizi ya Akili Mnemba katika utoaji haki Mahakama ya Rufani,’’amesema.
Ameeleza kuwa bila kufanya urekebishaji wa mchakato wa biashara (business process re-engineering) na kuhamia katika matumizi ya Teknolojia hawawezi kukabiliana na ongezeko la mashauri yanayotoka kwenye Mahakama za Mkazi kwenda katika Mahakama ya Rufani kwa kutegemea tu mpangilio wa kisheria, kanuni na idadi ya Majaji wa Rufani waliopo na idadi ya Majopo yaliyopo.
Amesema mkutano huo uwe mwanzo wa kuweka mikakati ya kuziangalia sheria, kanuni na kuzichakata upya urekebishaji wa mchakato wa biashara na taratibu za Mahakama ya Rufani na Mahakama za ngazi mbalimbali ili wamudu ongezeko la mashauri na kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi
“katika mkutano huu tutapokea na kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu mashauri katika Mahakama ya Rufani na kujaadili taarifa ya Msajili wa Mahakama ya Rufani kuhusu mafanikio tuliyoyapata katika usikilizaji wa mashauri na changamoto ambazo wamekutana nazo” amesema