Dkt. Deo Mwapinga amechaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kuidhinishwa kwa kauli moja na Maspika wa Mabunge wa Nchi Wanachama wa ICGLR.
Tukio hilo lmefanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa FP-ICGLR uliofanyika Luanda Angola Aprili 25, 2025.
Pamoja na tukio hilo, katika mkutano huo Wabunge wanaowakilisha mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu walikutana kujadili masuala ya amani, usalama na utawala wa kidemokrasia.
Katika hotuba yake mara baada ya kitangazwa kushika nafasi hiyo, Dkt. Mwapinga alitoa shukrani kwa nchi wanachama kwa heshima hiyo, na kuahidi kudumisha Malengo ya FP-ICGLR ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa wabunge katika ukanda wa maziwa Makuu.
“Hii sio tu heshima kwangu bali uthibitisho wa imani kubwa ambayo nchi wanachama wa ICGRL walionayo kwa Tanzania hususani katika kupambania maswala ya ulinzi na amani, ushirikiano wa kikanda na maswala ya demokrasia.
“Ninakubali jukumu hili kwa kutambua kazi iliyo mbele yetu ambayo ni kupigania amani na usalama, kuimarisha diplomasia ya kibunge, kukuza ushirikiano wa kikanda na kukuza utawala bora katika eneo letu.” Alisema Dkt. Deo.
Jukwa la Bunge la ICGLR linajumuisha Mabunge kutoka nchi 12 wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu likiwa na lengo la kusaidia utekelezaji wa itifaki iliyosainiwa mwaka 2006 katika kuimarisha, Ulinzi na Usalama, demokrasia, utawala bora na haki za binadamu