Na Janeth Raphael -MichuziTv SONGWE
IMEELEZWA kuwa Nchi ya Tanzania inazidi kuimarika kiuchumi kupitia uzalishaji wa gesi aina ya helium,inayotumika kwa ajili ya vipimo vya MRI,Scanners,pamoja na kuendeshea Roketi na Mitambo ya mawasiliano ya Anga.
Uzalishaji huo unatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya kukamilika kwa leseni za uchimbaji wa gesi hiyo,zinazotolewa na serikali,huku vibali vya uchimbaji vikiwa vimetolewa kwa kampuni ya Helium One
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea mradi huo Wilayani Momba Mkoani Songwe,Msimamizi wa mradi Emmanuel Gachucho amesema kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi wa chuo kikuu cha Oxfor,,Tanzania inakadiriwa kuwa na hifadhi ya zaidi ya futi bilioni 138 za ujazo wa gesi ya helium kiasi ambacho kinaweza kuiweka Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakuu duniani.
Gachucho amesema gesi hiyo inakwenda kuanza kuzalishwa hapa nchini mara baada ya serikali kusaini leseni za uzalishaji gesi hiyo baina yao na kampuni ya Helium One,ambao wapo tayari kuanza uzalishaji huo.
Amefafanua kuwa,uzalishaji wa gesi hiyo ambayo inapatikana katika bonde la ziwa Rukwa,itachangia kuongeza uzalishaji wa pato la taifa,lakini pia itasaidia kuinua uchumi.katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
“Tunatarajia kuanza kuzalisha gesi hii ya Helium ambayo huzalishwa katika nchi za nje,uzalishaji huo utasaidia uchumi wa nchi kupata katika maeneo mbalimbali,”alisema Gachucho.
Amesema gesi hiyo inayopatikana kwa nadra duniani ina matumizi muhimu katika teknolojia ya kisasa,huduma za afya,utafiti wa anga,na sekta za ulinzi ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja helium imekuwa kiungo katika maendeleo ya teknolojia ya hali ya juu.
Naye mjiolojia Venosa Ngowi kutoka Wizara ya madini,amesema,Tanzania imevutiwa na uwekezaji mkubwa katiika sekta ya utafiti na uendeshaji wa gesi ya helium,katika blonde la ziwa Rukwa,ambapo amesema moja ya kampuni inayojihusisha na na utafiti ni Hellium Global One.
Amesema moja ya faida itakayokwenda kupata nchi baada ya kuanza kuzalisha gesi hiyo ni kuboresha upatikanaji wa vifaa vya uchunguzi wa.magonjwa kama MRI,Ajira zitaongezeka.
Ngowi ameaema mrad huo unatarajia kuongeza fursa za ajira katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kuvutia wawekeza wa kimataifa kuja kuwekeza kupitia mradi huo katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo amesema uhusiano baina sekta ya madini na taasisi za elimu ya juu unaweza kuendeleza utafiti wa kisayansi na maendeleo ya kiteknolojia katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha amefafanua zaidi ya kuwa Tanzania inaweza kuwa kiungo muhimu katika kupunguza uhaba wa helium duniani hususani katika matumizi ya kimkakati katika sekta ya anga,Ulinzi.na Afya.
Kwa upande wake Meneja wa Madini Mkoa wa Songwe amesema mbali na Tanzania,mataifa mengine yanayozalisha gesi ya helium ni Marekani,Urusi,Qatar,Saudi Arabia na Algeria ambapo kwa pamoja nchi hizi zimeweka msingi wa soko la.kimataifa la helium.