Mchungaji Patrick Muthee kutoka nchini Kenya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki Wiki ya Uamsho na Kuliombea Taifa mara baada ya kupokea mualiko na kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutoka Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Haron Muturi kutoka nchini Kenya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijink Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki Wiki ya Uamsho na Kuliombea Taifa mara baada ya kupokea mualiko na kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutoka Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi Victor Chihimba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea wachungaji kutoka nchini Kenya kwaajili ya kushiriki Wiki ya Uamsho na Kuliombea Taifa mara baada ya kupokea mualiko na kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutoka Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
………..
WACHUNGAJI na Waimbaji kutoka Tanzania na Kenya wanatarajiwa kushiriki katika Wiki ya Uamsho na kuliombea Taifa ili kuendelea kuwa na Amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu ambapo mwaliko huo umetolewa na Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutokea Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 25, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mhubiri kutoka nchini Kenya Mchungaji Patrick Muthee amesema Watanzania na wanajumuiya ya Afrika Mashariki wanatakiwa kuendelea kudumisha amani na hasa kipindi hiki ambacho Taifa la Tanzania linaelekea katika Uchaguzi Mkuu.
“Tumekuja nchini Tanzania kuungana na ndugu zetu wa Kwaya ya Gethsemane pamoja na Kanisa Group Kinondoni (GGK)ambapo wameandaa wiki ya maombi mbalimbali ya kuliombea Taifa na kwa wakati huu kuomba amani,Umoja na mshikamano ni kipaumbele chetu kwani tunatambua Watanzania watakuwa na uchaguzi Mkuu mwaka huu.Hivyo tunawaombea wawe na amani.”
Pia Mchungaji Mwangi amesema Tanzania na Kenya wamekuwa na mahusiano ya karibu na undugu wao umekuwepo tangu wakati wanamfukuza mkoloni na kupata uhuru na hiyo imeipatia Kanisa kipaumbele kupeleka injili pamoja na kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni kinondoni na kiongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanashirikiana vizuri sana.
Amesema kutokana na hilo imetoa nafasi kubwa ya hata kupata wa wahubiri na waimbaji kutoka nchi hizo mbili pasipokuwa na vikwazo Wala matatizo yeyote na pia hata viongozi wa Serikali zote mbili wanashirikiana vizuri .
Kwa upande wake Mchungaji Harun Muturi Mwangi kutoa Naoribi Kenya amesema amekuja nchini Tanzania kwa mualiko wa Kanisa la Kinondoni Waadvetista Wasabo kwa ajili ya wiki ya uamsho na lengo ni kuamshana katika kumtukuza Mungu.
“Tunakuja kujiunga pamoja na waumini wenzetu na tutashiriki kwa maombi kwa ajili ya kuombea nchi hizi mbili na ulimwengu wote kwa ujumla.Pia tunaomba kwa ajili ya uchaguzi wa Tanzania unaokuja ili amani iweze kushamili,”amesema Mchungaji Harun
Ameongeza “Tunaombea Kanisa hili na nchi yote ya Tanzania na zaidi tunawashukuru Watanzania kwani wamekuwa watu wema na hawana vurugu na Mungu wetu awasaidie waendele kuwa hivi na wamuamini Mungu .”amesisitiza.
Awali Mwenyekiti wa Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) Samora Sadick amesema wanawiki nzuri ya maombi ya kuliombea Taifa na nyimbo za Injili ambazo zinahamasisha amani nchini kwetu.
“Hivyo tunawaalika watu wote ili kushiriki katika wiki hii kwa ajili ya kuimba pamoja na kufahamiana kwa pamoja ili Mungu ajapo kwa umoja waweze kulithi makao ya Mbinguni.”
Katika maombi hayo pia Kwaya ya Gethsemane pamoja na uongozi wa Kanisa hilo umewaalika wahubiri kutoka Kenya kwa ajili ya kuongoza mahubiri na maombi hayo yatakayofanyika kuanzia Jumapili ya Aprili 27 mpaka Mei 3 mwaka huu kuanzia saa 10 jioni kila siku.
Akizungumza wakati wa wa Wachungaji hao kutoka nchini Kenya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mchungaji wa Kanisa la Wasabato Mtaa wa Kinondoni Pastor Victor Chihimba amewakaribisha watu wote wa dini zote na madhehebu yote kwenye wiki hiyo maalumu itakayosheheni Mibaraka kupitia mahubiri.
“Kama Kanisa tunatambua umuhimu wa kukiweka Taifa letu la Tanzania katika mikono ya Mungu,hivyo katika wiki hiyo ya Maombi tunatarajia kufanya Maombi mbalimbali yenye kuliweka Taifa katika mikono yake Mungu na hatimaye kuifanya nchi kuendelea kuwa na amani ,upendo na mshikamano.”amesema.
Aidha Mchungaji Chihimba amesema kwaya mbalimbali zitakuepo kwa wiki nzima kuwabariki watu kwa njia ya nyimbo huku akitoa mwito kwa Watanzania wa madhehebu yote kushiriki katika juma hilo ili kuungana kwa pamoja katika Maombi mbalimbali yenye lengo la kuomba baraka kwa kila mmoja wetu. “Tukio hili la Maombi limekuwa linafanyika kila mwaka.”