Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 25, 2025 amewasili mkoani Mwanza ambapo ataelekea Nansio-Ukerewe kwa ziara ya siku moja.
Akiwa katika kisiwa hicho Mheshimiwa Majaliwa atakagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali yenye hadi ya Huduma za Rufaa ya Mkoa, ataweka jiwe la msingi la jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe pamoja na kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Getrude Mongela.