Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza waklati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Tume na Wadau wa Uchaguzi kutoka Halmashauri ya Singida Vijijini.
Wadau mbalimbali wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Singida Vijijini wakiwa katika mkutano huo leo Aprili 26,2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akijadili jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga wakati wa kikao hicho cha Tume na Wadau wa Uchaguzi kutoka Halmashauri ya Singida Vijijini.
Mbunge wa Singida, Kaskazini, Ramadhani Ighondo akizungumza kwaniaba ya madiwani na kuithibitishia Tume kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri ya Singida Vijijini kuwa walihitaji mabadiliko hayo yaendane na jina la eneo lao.
Wadau wa Uchaguzi kutoma Halmashauri ya Wilaya ya Singida weithibitishia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi juu ya nia yao ya kutaka kubadili jina la Jimbo la Singida Kaskazini kuwa Jimbo la Ilongelo.