Na Mwandishi Wetu
UBALOZI wa Tanzania nchini Namibia kwa kushirikiana na Chuo cha Triumphant wameandaa Kongamano la Kwanza la Kiswahili lililozungumzia mchango wa lugha ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika hususan Namibia.
Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo lililofanyika Aprili 25, 2025 alikuwa Lt.Gen.(Rtd) Epaphras Denga Ndaitwah, Mwenza wa Rais wa Namibia.
Mtoa mada Mkuu kutoka Tanzania alikuwa Bi.Consolata Mushi, Katibu Mtendaji wa BAKITA aliyemwakilisha Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na MichezoProf.Palamagamba Kabudi.
Watoa mada wengine kutoka Tanzania walikuwa Balozi Lt.Gen.(Rtd) Abdulrahman Shimbo, Balozi Brig.Gen.(Rtd) Francis Mndolwa na Dkt .Eliah Victor, Mkurugenzi wa Vipindi kutoka TBC.
Kwa upande wa Namibia,mtoa mada alikuwa ni mmoja wa Wapigania Uhuru wa Namibia aliyeishi Kongwa, Dodoma nchini Tanzania.
Aidha ,Kongamano hilo lilihudhuriwa wa Wapigania Uhuru wa Namibia walioishi Tanzania,Vijana wa Namibia waliozaliwa uhamishoni, Mabalozi, Wanazuoni,Wanafunzi pamoja na Waandishi wa Habari.