Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa ameongozana na Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa katika mazungumzo mafupi na Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, baada ya kumpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipitia baadhi ya taarifa alizokabidhiwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, wakati alipoongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri Bw. Twaha Mwakioja.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akisalimiana na Bw. Chu Kun, Kansela wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, alipowasili kwa ajili ya kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam).
……..
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe April 26 hadi 29, 2025.
Katika ziara hiyo inatarajiwa kuwa na vikao mbalimbali vya majadiliano kati ya ujumbe wa Tanzania na China, yanayolenga kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.