Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI MKUU,Mhe. Kassim Majaliwa,amewataka wakulima na wananchi kwa ujumla wahakikishe wanajiunga na vyama vya ushirika vilivyosajiliwa, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo leo Aprili 27, 2025 wakati akifungua mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
“Wadau wote wa maendeleo, endeleeni kushirikiana na Serikali katika kutoa rasilimali, utaalamu na ubunifu unaohitajika katika kuendeleza sekta hii muhimu.”amesema Mhe.Majaliwa
Aidha ameitaka Wizara ya Kilimo kuhakikishe maandiko ya taarifa zilizozinduliwa zinaandaliwa pia kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika nazo.
Pia Waziri Mkuu amesema Sekta ya Ushirika nchini inaendelea kuimarika kwa kasi, ikiwa ni mhimili muhimu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hasa katika maeneo mbalimbali.
“Hadi sasa, Tanzania inajivunia kuwa na zaidi ya vyama 7,000 vya Ushirika vilivyosajiliwa, vyenye jumla ya wanachama zaidi ya milioni nane. Vyama hivi vinajumuisha sekta mbalimbali za uchumi kama vile kilimo, uvuvi, madini, biashara na huduma za kifedha.”
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua madhubuti za kuleta mageuzi katika Sekta ya Ushirika ikiwemo kuboresha mifumo ya usimamizi na uendeshaji wa vyama vya ushirika pamoja na kuimarisha masoko ya mazao kupitia mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
“Kuwapatia Maafisa Ushirika vitendea kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kuboreshwa kwa upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika na kuimarishwa kwa huduma za kifedha kupitia kuanzishwa kwa Benki ya Ushirika (COOP Bank).”
Aidha Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iimarishe na kufanya ufuatiliaji wa Watendaji wa Vyama vya Ushirika ili wazingatie maadili ya utumishi wa ushirika, uwazi, uwajibikaji na utawala bora, na hivyo kuwavutia wanachama na wawekezaji.
Pia, Mhe. Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo, pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, iharakishe na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mikakati yote iliyopitishwa, hususan katika maeneo ya teknolojia ya kilimo, upatikanaji wa pembejeo, na masoko ya mazao
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzisisitiza taasisi za kifedha, zikiwemo benki na mifuko ya maendeleo, ziendelee kushirikiana kwa karibu na vyama vya ushirika kwa kuweka mifumo rafiki ya upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa wakulima na wafanyabiashara wadogo.
Akizungumzia uzinduzi rasmi wa mradi wa Mashamba Makubwa unaofadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania, Waziri Mkuu amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya BBT.
“Mradi ambao nimeuzindua leo, utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030. Gharama ya jumla ya utekelezaji wa BBT Project 1 ni Dola za Marekani milioni 241.27, ambapo AFDB itachangia Dola milioni 129.71, sawa na asilimia 53.76 ya gharama hiyo. Serikali ya Tanzania itachangia asilimia 46.24 ya mahitaji hayo ili kukamilisha mradi huu.”
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo,Me. Hussein Bashe amesema ushirika ni njia pekee inayowajengea uimara wanaushirika na kwamba benki ya ushirika inakwenda kurahisisha malipo ya wakulima. Benki ya Ushirika inamtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 50 na itakuwa na mawakala zaidi ya 50 nchini.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Ushirika (Coop Bank), Profesa Gervas Machimu amesema benki hiyo itakuwa nguzo ya maendeleo ya ushirika mijini na vijijini, itarudisha heshima ya ushirika na kuchochea uchumi wa wananchi.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Tume ya Vyama vya Ushirika, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya Ushirika itaendeshwa kisasa zaidi na itakuwa na ushindani na kutoa taswira ya ushirika wenye tija.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shoroba za Kilimo Groffrey Kirenga, alipozindua ramani ya Mpango wa Shoroba za Kukuza Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kuzindua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Tabora (WETCU 2018 ltd) Samweli Jokeya kuhusu Majani ya Tumbaku ya Mvuke, wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kuzindua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Majid Nsekela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Igembensabo Christian Mkude kuhusu zao la Dengu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kuzindua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Majid Nsekela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mhasibu wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama Hamis Hussein kuhusu zao la Pamba wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kuzindua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Majid Nsekela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu ramani ya Mpango wa Shoroba za Kukuza Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kuzindua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shoroba za Kilimo Groffrey Kirenga, alipozindua.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023 na 2023/2024, wakati wa uzinduzi wa Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha Ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023 na 2023/2024 baada ya kuizindua, wakati wa Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha tuzo aliyokabidhiwa ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya ushirika, wakati wa uzinduzi wa Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika, Aprili 27, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri wa Kilimo Hussein Bashe,akizungumza wakati wa mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 leo Aprili 27,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 leo Aprili 27,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Tume ya Vyama vya Ushirika, Abdulmajid Nsekela,akielezea lengo la Mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 leo Aprili 27,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mdahalo wa upatikanaji Mitaji ya Fedha na Fursa za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 leo Aprili 27,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.