Afisa Habari Mkuu,kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Joyce Mgaya,akizungumza na watoto Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam mara baada ya kuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya ziara ya mafunzo pamoja na kutembelea Mji wa Serikali Mtumba ziara ya mafunzo iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Na.Alex Sonna-DODOMA
WATOTO Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam wametembelea Mji wa Serikali Mtumba Dodoam huku wakiushukuru Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) kwa kudhamini ziara ya mafunzo kwa kutumia reli ya kisasa (SGR).
Akizungumza leo Aprili 29,2025 kwa niaba ya BRELA, Afisa Habari Mkuu, BRELA Bi. Joyce Mgaya amesema ziara hiyo in aonesha dhamira ya BRELA katika kusaidia makundi yenye uhitaji maalum.
“Mtendaji Mkuu wetu aliona ni jambo jema kuwapa watoto hawa fursa ya kutembelea makao makuu ya nchi na kujionea miradi ya maendeleo inayotekelezwa,” amesema Bi Mgaya.
Hata hivyo ameongeza kuwa kwa wengi wao,ni mara ya kwanza kupanda treni ya SGR na kufika Dodoma, na kwamba ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya BRELA kusaidia jamii kupitia programu mbalimbali za kuwafikia wananchi.
Aidha Bi.Mgaya ametoa wito kwa Taasisi zingine ziendelee kuwakimbilia watu wenye mahitaji Kwa kuhakikisha wanawasaidia mahitaji mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo cha TUYATA, Bi Fauzia Jabir amesema kuwa wanaishukuru BRELA kwa safari hiyo kwani watoto wengi wamefurahi na katika maisha yao hawajawahi kupanda treni.
“Watoto wamefurahi mno, jambo hili halijawahi kutokea. BRELA imefanya jambo kubwa kwa kusimama na watoto hawa wahitaji. Wamehamasika kusoma zaidi baada ya kuona uzuri na fursa zilizopo nchini,” amesema Bi Jabir.
Hata hivyo, ameeleza kuwa licha ya mafanikio ya kielimu waliyonayo, kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kubwa ya makazi kwa watoto yatima, na hivyo kuomba msaada wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa watoto na wajane.
Mmoja wa walionufaika na kituo hicho, Bi Ayman Jaffar Abubakar ambaye pia ni msemaji wa TUYATA, amesema kulea watoto kutoka mazingira mbalimbali si kazi rahisi lakini kwa neema ya Mungu, wanajitahidi kutoa malezi bora na kuwaelekeza katika njia sahihi.
“Watoto wengi wanaishi kwa walezi, hivyo ni changamoto kuwafuatilia kikamilifu. Tunaishukuru BRELA kwa kutuunga mkono na tunaomba waendelee kuwa nasi hadi tufikie malengo yetu,” amesema




WATOTO Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam wakiwa ndani ya reli ya kisasa (SGR) kuja jijini Dodoma kutembelea Mji wa Serikali Mtumba ziara ya mafunzo iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

WATOTO Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam wakishuka ndani ya reli ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili jijini Dodoma kutembelea Mji wa Serikali Mtumba ziara ya mafunzo iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).


Afisa Habari Mkuu,kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Joyce Mgaya,akizungumza na watoto Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam mara baada ya kuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya ziara ya mafunzo pamoja na kutembelea Mji wa Serikali Mtumba ziara ya mafunzo iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).


Watoto Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam wakifurahia Mji wa Serikali Mtumba baada ya kutembelea ziara ya mafunzo iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).


Afisa Habari Mkuu,kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Joyce Mgaya,akizungumza na waandishi ya habari jijini Dodoma mara baada ya kudhamini ziara ya mafunzo ya Watoto Yatima na wenye Ulemavu 100 kutoka Kituo cha Kulelea Yatima cha Tulee Yatima Tanzania (TUYATA) kutoka Dar es Salaam mara baada ya kutembelea Mji wa Serikali Mtumba ziara iliyodhaminiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo cha TUYATA, Bi Fauzia Jabir,akiishukuru BRELA kwa safari hiyo kwani watoto wengi wamefurahi na katika maisha yao hawajawahi kupanda treni.

Mmoja wa walionufaika na kituo cha TUYATA na msemaji wa TUYATA Bi Ayman Jaffar Abubakar,akielezea historia yake kwa waandishi wa habari.