Na Belinda Joseph-Songea DC.
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Peramiho kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi. Elizabeth Gumbo, leo tarehe 29 Aprili 2025, amefungua rasmi mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika Ukumbi wa Jenista Mhagama uliopo katika Shule ya Sekondari ya Maposeni.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bi. Gumbo amesema: “Ni matumaini yangu kuwa, kupitia semina hii, kila mshiriki atapata uelewa wa kutosha utakaomwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kufanikisha zoezi hili muhimu.”
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo washiriki kuhusu mbinu bora za kujaza fomu, matumizi ya Mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura (Voters Registration System), pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya kuandikisha wapiga kura.