LEO Aprili 29, 2025, wanachuo na wakufunzi wao kutoka Chuo Kikuu Cha Whitworth cha Marekani, wametembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid.
Pamoja na mambo mengine, wanachuo hao wanaosoma masomo ya siasa, falsafa na uhusiano kimataifa, walitaka kupata ufahamu juu ya masuala ya demokrasia, sera za CCM kuhusiana na watu wenye ulemavu, miundombinu na maendeleo ya watu kwa ujumla
Wanachuo hao wapo nchini kwa kushirikiana na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni, Dar es Salaam kujifunza utamaduni wa Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja na mafunzo kwa vitendo.