Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ghati Memorial iliyoko Mkoani Singida wametembelea Banda la TARURA kwenye Maonesho ya OSHA yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mandewa.
Wanafunzi hao wamesema wana ndoto ya kuwa Wahandisi hivyo wameona ni vyema kutumia fursa ya maonesho hayo kufika TARURA na kujifunza.