:::::::::
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Yaibuka Mshindi wa Kwanza Katika Maonyesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma katika Maonyesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni yaliyofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Aprili, 2025 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
TEA ilikuwa miongoni mwa taasisi zaidi ya 30 zilizoshiriki katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni, kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza shughuli za kitamaduni nchini.
Vigezo vilivyotumika katika kutoa tuzo hizo ni pamoja na muonekano wa banda, utoaji wa huduma kwa wageni waliotembelea banda, pamoja na muda wa kufungua na kufunga huduma.
Tuzo hizo zilitolewa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Prof. Paramaganda Kabudi, ambaye alipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwa mchango wao katika kufanikisha maonyesho hayo.