Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa :Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewahukumu kunyongwa hadi kufa wanaume watatu kwa makosa ya mauaji ,adhabu hiyo imetolewa kwa washtakiwa hao wote baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia katika nyakati na maeneo tofauti ya wilaya ya sumbawanga .
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa kamishana msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi SACP Shadrack Masija amewataja watu hao kuwa ni Devi Palasido Mwanalinze (25) mkazi wa makutano ,huyuo alitena kosa la kumuua kwa kukusudia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka (32) mkazi wa sumbawanga Asilia tarehe 14/02 /2024 saa 02:00 usiku wakati mwanamke huyo akitoka kanisani kwenye ibada ya jumatano ya majivu .
Wakati wa kusikiliza kesi yake ilibainishwa kuwa Devi alimuua mwanamke huyo baada ya kuwa amembaka na kumpora simu yake na adhabu hiyo imetolewa tarehe 25/4/2025.
Wakati huo huo Charles Kashinje (48) mkazi wa kapenta wilaya ya sumbawanga vijijini naye amepewa adhabu hiyo baada ya kumuua mwanamke aitwae Kija Lutema Kasiwa (35) mkazi wa kijiji cha kapenta wilaya ya sumbawanga tarehe 28 /4/2025 adhabu hiyo imetolewa 25/4/2025 ,chanzo ni mgogoro wa shamba .
Mwingine ni Sanyiwa Nyorobi Mtemasho (47) mkazi wa kilangawana wilaya ya sumbawanga huyo alimuua Tiga Washa (27) mkazi wa eneo la kilangawana tarehe 18/12/2023 majira ya saa saba usiku kutokana na mgogoro wa shamba adhabu yake ilitolewa 4/3/2025 .
Adhabu zote hizo zimetolewa naMhe. Joseph D. Luambano hakimu mkazi mfawidhi (Extended Jurisdiction) wakati akitoa adhabu hizo amesisitiza kuwa ziwe fundisho kwa watu wengine.
Jeshi la polisi mkoa wa Rukwa linatoa wito kwa wananchi kuacha tamaa ya ngono na mali pia kutatua migogoro yote kwa kufuata sharia na taratibu za nchi.