Katika kuadhimisha siku ya wafanya kazi yaani Mei Mosi Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa mara limewaasa watumishi wa wote kuwa sehemu ya Mkakati wa uhamasishaji wa matumizi Bora ya Nishati Safi ya kupikia ya Umeme.
Kauli hiyo imetolewa katika mashindano ya mei Mosi Mkoani mara na Afisa uhusiano na huduma kwa wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TENESCO) Mkoani Mara Bi.Joyce Wiliam Wakati akitoa Taarifa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa mara Kanali Evans Mtambi baada ya kutembelea Banda la Shirika hilo.
“Nishati Safi nirahisi kutumia kutunza Mazingira naninafuu na kuokoa Muda hasa kwa watumishi”Alisema Bi.Joyce William.
Katika hatua nyingine Bi.joyce Shirika hilo limeanzisha namba kwa huduma na kwa wateja bila malipo ambayo 180 ikiwa nikurahisisha kwa wateja Kutoa Taarifa Bure bila malipo na kutatua changamoto za wateja kwa Wakati wanazo kutana nazo.