Jukwaa la kwanza wakuu wa taasisi za umma Zanzibar kuanza Mei 11
Zanzibar. Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar imeandaa jukwaa la kwanza la wakuu wa taasisi za uwekezaji wa umma litakalofanyika kwa siku tatu; Mei11-13, 2025 katika hoteli ya Golden Tulip Airport iliyopo visiwani humo.
Msajili wa Hazina Zanzibar Bw. Waheed Mohammad Ibrahim Sanya alisema Jumamosi, Mei 3, 2025 kuwa lengo kuu la jukwaa hilo ni kuwaunganisha wakuu wa taasisi kutoka taasisi mbalimbali za umma ili kujadili changamoto za pamoja, kubadilishana uzoefu, na kuanzisha mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji wa taasisi zao.
“Kupitia jukwaa hili, wakuu wa taasisi za umma wataweza kuimarisha ushirikiano, kubadilishana maarifa, na kuchochea ubunifu,” alisema huku akitabanaisha kuwa mgeni rasmi atakuwa Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Kaulimbiu ya Jukwa hilo ni “Uongozi Bunifu na Mashirikiano ni Muhimu ili kufikia Maendeleo Endelevu Zanzibar.”